KINGA DHIDI YA SARATANI
Nkukurah, D. K
nkukurahd@yahoo.com , nkukurah blogspot.com
Tafsiri ya neno saratani
Saratani ni mgawanyiko
mbaya wa uzalishaji na usambaaji wa chembe chembe hai zisizo za kawaida
ndani ya mwli.
Aina kuu za
saratani:
Saratani ya mapafu
Saratani ya ngozi
Saratani ya shingo ya uzazi kwa
wanawake
Saratani ya matiti kwa wanawake
Saratani ya tezi dume
Saratani ya matumbo
Saratani ya midomo kwa wavuta sigara
Viashilia
hatarishi:
C – Mabadiliko katika
upatikanaji wa haja kubwa
A – Vidonda visivyopona
U –Kutokwa na
damu/majimaji/usaha usiokuwa wa kawaida
T –Uvimbe kuwa mgumu au
kuongezeka kwa ukubwa
I –Shida ya kusaga chakula
tumboni au kumeza
O –Mabadiliko ya wazi kwa uvimbe
uliokuwa nao siku nyingi
N –Kikohozi kisumbufu au sauti
kukwaruza
Visababishi
Vikuu:
1. Mionzi
2. Kemikali
3. Baadhi ya Bakteria na Virusi
4. Chakula (Fangasi na
Additives)
5. Tumbaku na sigara
6. Pombe
Visababishi hivi
vikuu husababisha uokisidishaji wa molekuli za mwili na kuzifanya kuwa radikali
huru. Radikali huru uanzisha mapambano dhidi ya molekuli zingine na kuzifanya
kuwa radikali huru pia. Mchakato huu ukiendelea bila kudhibitiwa mapema
utengeneza radikali huru nyingi mwilini ambacho hugeuka kuwa chembechembe za
saratani. Angalia mchoro huu hapa chini.
Kudhibiti mchakato wa
uokisidishaji
Ili kudhibiti mchakato wa uokisidishaji ni kukubali kula
vyakula vyenye vipinga uokisidishaji. Vyakula hivi ni vyepesi na rahisi, pia
vinapatikana katika mazingira yetu ya kawaida kwa bei nafuu. Kwa kufanya hivyo
utakuwa umejiweka katika mazingira mazuri ya kujikinga dhidi ya saratani.rejea
jaribio dogo lililofanywa kuthibitisha uokisidishaji kwenye tunda la epo
lililopasuliwa katikati, upande mmoja kupakwa maji ya limao yenye wingi wa
vitamin C na upande mwingine kuachwa wazi na kuruhusu uokisidishaji kutokea.
Ifuatayo chini ni orodha ya
vipinga uokisidishaji:-
1.
vitamin
Vitamin A: Vyanzo vikuu; Karoti, skwashi, brokoli, viazi
vitamu, nyanya, boga, pichi na aprikoti
Vitamin C: Vyanzo vikuu; machungwa, limao, chenza, embe , nanasi,
ndizi, epo, pilipili za kijani, brokoli, mboga za kijani, strobeli na nyanya,.
Vitamin
E: Vyanzo vikuu; mbegu (Nuts and seeds), nafaka, mboga
za kijani
2.
Madini ya Selenium
Vyanzo
vikuu; samaki,
mtama,mayai, na vitunguu shwaumu
3.
Kemikali za mimea
Kemikali ya Flavenoids
. Vyanzo vikuu; Maharage, zabibu za zambarau, komamanga,kreni beli, chai
Kemikali
ya Lycopene. Vyanzo vikuu; Nyanya, barungi za pinki, na
tikiti maji
Kemikali
ya Lutein. Vyanzo vikuu; mboga za majani mfanoo; brokoli,
na spinachi
No comments: